Sunday, July 03, 2005

Wabunge wamekataa kuifunda serikali

Na Nikita Naikata

SITAKI kuona Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanialiko tupu. Wabunge hawamo. Waliomo ni wa kuokoteza.
“Nikae pale ili iweje? Wenzangu wananichafuliajimboni. Nikikaa hapa ina maana nimekata tamaa nasitaki kuingia katika ushindani,” amesema mbunge mmojaaliyekuwa akipanda ndege kwenda mkoani kwake.
Na hii ni kawaida. Mkutano wa mwisho wa Bunge ambaohuwa wa bajeti inayofuatiwa na uchaguzi mkuu, huwa nawabunge wachache. Lakini huu ni wakati wa bajeti. Ni wakati wakuwasilisha mapato na matumizi ya serikali katikanyanja mbalimbali. Ni wakati muhimu sana wa kujadiliafya ya uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.
Tatizo ni kwamba wabunge wote wanadai kuwa kuwa“bize.” Ama wanapitapita majimboni kukamilisha ahadi;au wanajenga hoja mpya za kutekeleza yale ambayohawakuwahi kutekeleza, au wanapeleka lugha mwafaka kwawapiga kura wapya.
Na tayari, Rais Benjamin Mkapa, Tume ya Taifa yaUchaguzi na Cgham Cha Mapinduzi (CCM) wamesema kwambawengi waliojiandikisha kupiga kura mwaka huu nivijana. Ndiyo msingi wa “tuwape vijana kijana,” ambayo inakaribia kuwa “sera” ya CCM.
Kila mbunge hivi sasa anawinda vijana. Wako majimboniwakiwasaka na kuwaahidi kwamba “wakati wenu ni huu!”Wanawaahidi ajira na biashara!Nao vijana waliohamasika hawataki kusikiliza la mtumwingine. Wanataka ajira. Wanataka kusikiliza nakusikia lugha ya ajira. Na hakika wamejiandikishakweli.
Bali sokoni Mbagala Rangi 3 kuna hoja tofauti. Waulizevijana: Wanasema vijana mmejiandikisha wengi kupigakura mwaka huu? Kwa nini imekuwa hivyo? Jibu linatoka haraka, “Nani kakwambia tunataka kupigakura? Mbona tumekuwa tukipiga kura kila baada ya miakamitano na hakuna chochote tunapata? Sisi tumechukua vile vipande ili wasiwe wanatusakama kwamba hatuna vitambulisho!”
Kwa hiyo, bunge liko tupu kwa kuwa wabunge wanawasakawapiga kura kwa ajili ya kura za maoni na UchaguziMkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. Wanawasaka vijanawanaoteleza kama kambale. Kwa hali ilivyo, vijana wataendelea kuteleza.
Angalia duara hili la maangamizi: Bunge halina wabunge. Wabunge wanasaka wapiga kura ambao wengi waoni vijana. Wabunge hawako bungeni kujadili mambo yanayowahusu vijana katika kila wasilisho la wizara.
Na vijana wanasema wamejiandikisha kwa wingi iliwapate vitambulisho!Nani anamdanganya nani? Nani asiyejua kwambaHalmashauri za Wilaya zilishindwa kutenga asilimiatano kwa ajili ya maendeleo ya vijana? Nani hajui kwamba hakuna uwakilishi wa vijana katika mabunge yawilaya – zile kansili?
Nani hajui kwamba vijana wamekuwa wakitumiwa kamachambo tu katika siasa na zoezi la uchaguzilinapomalizika wanakimbiwa kama wenye ugonjwa wakuambukiza? Nani hajui kwamba chama cha wabunge vijana ni kwaajili yao wenyewe bungeni na si vijana walio nje yabaraza la kutunga sheria?
Hivi vikundi vingi navyovinaweza kupumbaza!Na wakati huu wa bunge la bajeti, wakati wabunge wengi hawamo barazani ndiyo wakati mzuri wa mawaziriwababaishaji kuleta chochote, kubwaga bungeni nakuondoka.Katika miaka ya karibuni, Bunge liliunda kamati zaidiza kudumu.
Hii ni kuwezesha kamati kujadili mambo yoteya serikali yanayofikishwa bungeni. Bajeti za wizara nazo pia huwa zimechambuliwa katika ngazi ya kamatiili kupunguza mzigo wa kuzijadili.Bali hili haliwezi kuhalalisha bunge kuwa “tupu” etikwa kuwa kamati ziliishajadili hoja za wizara.
Kamati zina wajumbe wachache; na mawazo maridhawa yawezakutoka nje ya kamati husika au idara ya serikali. Sitaki kuambiwa kwamba sharti wabunge wakimbie barazamuhimu la mwisho wa awamu yao kwa kisingizio chamaandalizi ya kurejea bungeni. Sitaki utaratibu unaoruhusu wabunge wakimbie wajibukwa madai kwamba wanapigania viti vyao.
Na serikaliyetu si nyoofu. Uwazi na ukweli unakuwa mdomoni kulikokatika vitendo.Wakati wabunge wamekimbilia majimboni na kuachashughuli kuu ya bajeti inaendelea, unakuwa wakatimwafaka kwa serikali kuingiza inachotaka na bilakukaguliwa.
Serikali ni mtoto mtukutu. Inahitaji kusimamiwa wakatiwote; kukemewa na wakati mwingine kufundwa kwa“bakora” ya wananchi wanaoiajiri. Sasa kamawawakilishi wa wananchi hawako bungeni, nani atafanyakazi hii?
Na si kwamba rais hajui hili. Si kwamba serikalihaijui hayo. Si kwamba Spika haoni hilo. Hapana. Wotehao wanafurahia kutokuwapo macho, masikio na mtima wawananchi ili waweze kufanya watakavyo. Sitaki kuona wabunge wakikimbia wajibu wao wakati badowako katika ajira ya wananchi.

MAKALA HII ILICHAPISHWA KWA MARA YA KWANZA KATIKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA JUMAPILI, JULAI 3, 2005, KATIKA SAFU YAKE YA SITAKI. Mwandishi wake anapatikana kwa barua pepe hii: nikitanaikata@yahoo.com